Tanzania Scholars Volunteer
Foundation

TSV FOUNDATION CONDUCTS MOTIVATIONAL VISIT AT URAFIKI SECONDARY SCHOOL TO INSPIRE STUDENTS AND STRENGTHEN PARTNERSHIPS

 

Tarehe 8 Oktoba, 2025 Uongozi wa shirika Umefanya Ziara ya hamasa katika shule ya Sekondari Urafiki iliopo wilaya ya Ubungo-Dar es salaam. 


Ziara hio ililenga kuweka uhusiano mzuri kati ya shirika na shule ya Sekondari Urafiki pia dhumuni kubwa la ziara lilikuwa kutoa hamasa na elimu wezeshi kwa wanafunzi wa madarasa ya Mitihani yaani kidato cha pili na Kidato cha nne. 

Mkuu wa shule Madam. Magdalena Sanga aliukaribisha uongozi wa shirika kwa furaha katika shule yake na kupongeza jitihada za shirika, pia alishauri uongozi wa shirika kuwa wabunifu na kufanya mambo makubwa zaidi nje ya elimu. 

Pia Mwenyekiti wa shirika Mhe. Juma Hamisi alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa shule kwa ujumla kuwa na ushirikiano na shirika ambao unalenga kuleta mabadiliko chanya. 

Kupitia ziara hio Shirika liliweza kuwapa wanafunzi mbinu bora za kufaulu mitihani ya umahiri, kuwaeleza mambo ya msingi ambayo wanafunzi wanapaswa kufanya kwa sasa ili kufikia malengo yao ya kujiendeleza kielimu katika ngazi za juu za elimu. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.