"PATHWAY TO SUCCESS, EMPOWERING LEARNERS FOR EXCELLENCE "[PSELE PROJECT]
UJUE MRADI WA NJIA YA MAFANIKIO, KUWAWEZESHA WANAFUNZI KWA UBORA
1.0 UTANGULIZI
Shirika la Wasomi la Kujitolea Tanzania, TSV FOUNDATION limeandaa mradi wa Mwaka mmoja,2025/2026 unaofahamika kwa kifupi [PSELE]. Katika mradi huo TSV FOUNDATION ndio inajukumu la kusimamia utolewaji wa Programu mbalimbali kupitia mradi huu.
1.2 PROGRAMU AU SHUGHULI ZA MRADI
Programu au shughuli za Mradi zinaendana na vipaumbele vya Sera ya nchi kupitia Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia, Taasisi ya elimu nchini pamoja na jamii nzima ya Kitanzania.
1.2.1 Huduma za mafunzo wezeshi ya Kimkakati.
Shirika limeandaa programu hii ya mafunzo wezeshi kwa Wanafunzi hasa katika vipindi vyao vya likizo pamoja na mda wao wa ziada nje ya ratiba ya shule kwa gharama ya chini sana ili kuwasaidia vijana wa kitanzania na jamii kwa ujumla [ TUITION CENTRE].
1.2.2 Programu za maandalizi ya Mitihani ya Taifa.
Shirika limeandaa programu hii kwa Wanafunzi wanaotamani kufanya vizuri zaidi hasa kwa mda mchache uliosalia kufanya mitihani yao ya taifa, ambapo programu itajikita katika mahitaji ya Mwanafunzi husika, udhaifu wake katika malengo yake pamoja na kumpatia mbinu za kumuandaa kikamilifu katika maandalizi ya mitihani ya taifa. [TACTICAL NATIONAL EXAMINATION PREPARATIONS].
1.2.3 Mitihani ya pamoja ngazi ya Shule na mwanafunzi binafsi.
Programu hii inalenga kuwakutanisha wanafunzi wa shule tofauti tofauti katika mitihani ya pamoja ambayo itawasaidia kujitathmini wao binafsi. Pia programu hii inalenga kuwapa wanafunzi uzoefu wa kuikabili mitihani ya umahiri. [STUDENTS JOINT EXAMINATIONS]
1.2.4 Uchapishaji na utoaji wa nyenzo za ujifunzishaji kama Package, Mitihani,Notes etc
Shirika litatoa nyenzo za ufundishaji mbalimbali kama vitabu, maswali & ufafanuzi wake, kazi za nyumbani kwa Wanafunzi wakati wa likizo, usahihishaji wa mitihani ya shule/taasisi yoyote. [DISTRIBUTION OF LEARNING AND TEACHING MATERIALS SUCH AS PACKAGE OF QUESTIONS, PASTPAPERS & NOTES]
1.2.5 Semina elekezi hasa kwa Watahiniwa.
Shirika litafanya ziara na semina elekezi kwa Wanafunzi wa shule mbalimbali hasa Watahiniwa kwa kuwashauri na kubadilishana mawazo juu ya maandalizi bora na muhimu katika mitihani yao ya taifa. Pia kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo kuwasisitizia kusoma kwa bidii pia kuwapa mbinu mpya za ujifunzaji.
2.0 MALENGO YA MRADI
Lengo kuu la mradi huu ni kuinua ubora wa elimu kwa kukuza na kuinua ufaulu wa Wanafunzi.
2.1 MALENGO MAHSUSI
Malengo Mahsusi ya mradi huu ni pamoja na,
a) Kuongeza ufaulu katika shule zenye ufaulu wa chini.
b) Kuwachochea wanafunzi katika kuipenda elimu na kusoma kwa bidii.
c) Kutekeleza kauli mbiu ya shirika "Elimu bora, haki ya kila Mtanzania".
d) Kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye Familia zenye kipato cha chini kupata elimu bora.
e) Kuandaa taifa la Wasomi mahiri.
3.0 MATARAJIO YA MRADI
Mradi unatarajia kuleta mageuzi ya kitaaluma kwa vitendo na kubadilisha hali ya ufaulu wa Wanafunzi katika mitihani ya taifa, kupunguza gharama na vikwazo vya kitaaluma kwa kutoa elimu bora kwa gharama nafuu ambazo kila mtanzania anaweza kugharamia pia kuimarisha taasisi za elimu kama shule za serikali na Binafsi zenye ufaulu wa chini kwa Wanafunzi ili kukabiliana na ushindani na kuwa msingi thabiti wa mabadiliko chanya katika sekta ya elimu nchini.
4.0 WALENGWA WA MRADI
Mradi unayagusa makundi manne (4) ambayo ni,
4.1 WANAFUNZI
Mradi huu unatoa fursa kwa Wanafunzi kujifunza na kuboresha ufaulu katika taaluma zao, pamoja na kukuza uhusiano chanya na Wanafunzi wengine kupitia mda wao wa ziada nje na ratiba ya shule/Taasisi.
4.2 TAASISI/SHULE
Mradi huu unatoa fursa kwa shule/Taasisi kupokea nyenzo mbalimbali za Kujifunzia kama Package za wanafunzi kila likizo au mapumziko mafupi ya Wanafunzi, Notes, Semina elekezi pamoja na Fursa ya kuwapima wanafunzi wake na wanafunzi wa shule/taasisi nyingine kusaidia kufanya tathmini ya shule.
4.3 HALMASHAURI HUSIKA
Mradi huu unatoa fursa kwa Halmashauri mbalimbali kuchochea ufaulu katika shule zao, kwa kuingia makubaliano na shirika katika kuchochea ufaulu wa shule zao, Pia Mradi huu unatoa fursa kwa Halmashauri mbalimbali kuajili walimu wa kujitolea wenye uzoefu
wa ufundishaji hasa katika shule zenye uchache wa Walimu katika Halmashauri husika.
4.4 SHIRIKA
Mradi huu unatoa fursa kwa Wanachama wa shirika kukuza uzoefu wa taaluma zao za Ualimu, Kuwaonganisha Walimu na Shule/Taasisi zenye uhaba wa walimu, Kuwaunganisha na Halmashauri mbalimbali zenye lengo la kuajiri walimu wa kujitolea.
5.0 MBINU NA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MRADI
Mradi huu utajumuisha mbinu mbalimbali ambazo zitakuwa na tija kubwa katika utekelezaji wa mradi pamoja na kufikia malengo ya Shirika, mbinu hizo ni;
a) Uwajibikaji, kujitoa na moyo wa dhati wa kulipambania shirika na Jamii kwa ujumla.
b) Kupata mazingira rafiki ya kutekeleza mradi
c) Kupata vifaa muhimu vya kitaaluma ambavyo vitasaidia kuchochea ujifunzishaji.
d) Kuwa na Ofisi binafsi itakayotumika kuwaunganisha walengwa wote wa mradi.
e) Kuwa na walimu sahihi wenye Kuzingatia misingi na itifaki za kitaaluma na watakao weza kufuaata kanunu, sheria na taratibu za mradi na eneo husika la utendaji kazi wa mradi .
f) Walimu mahiri katika ufundishaji
g) Kuandaa semina na ziara maalumu kwa Wataalamu wa elimu zenye lengo la kukuza ubobevu na umahiri kwa walimu wa mradi hasa kuendana na mabadiliko ya sekta na Sera ya elimu.
h) Kuwachochea usawa wa kijinsia hasa katika utekelezaji wa mradi.
i) Kuhudumia walengwa wote bila kujali nafasi, Hali ya kiuchumi, jinsia, dini, kabila wala eneo.
j) Uadilifu na uzalendo kwanza Maslahi baadae.
6.0 UKUSANYAJI WA MICHANGO, UHIFADHI WA PESA ZA MRADI NA MALIPO YA WATUMISHI WA MRADI
Pesa zote kupitia mradi huu zitakusanywa na kuhifadhiwa kupitia akaunti ya Benki ya shirika AKAUNTI YA NMB 20810067031 yenye jina TANZANIA SCHOLARS VOLUNTEER FOUNDATION.
6.1 Ukusanyaji wa Michango kwa Wanafunzi na Wadau Binafsi
Michango yote itakusanywa kupitia akaunti ya Benki ya shirika ambayo itafafanuliwa kwenye fomu ya usajili wa wanafunzi.
6.2 Malipo ya pesa kwa Watumishi wa Mradi
■Walimu; malipo yao yatafanyika kwa awamu mbili mwanzo wa programu na mwisho wa programu kupitia ofisi ya Mhasibu wa Shirika.
■Mahali; gharama ya eneo ita lipwa mwanzo wa programu husika kupitia ofisi ya Mhasibu wa shirika.
■Wasimamizi wa Programu: malipo ya wasimamizi wote wa programu yatalipwa kwa awamu mwanzo wa mafunzo na mwisho wa mafunzo.
