Tarehe 27.03.2026, Taasisi ya Elimu Tanzania - TET : Mwenge - Dar es salaam.
Shirika la Wasomi la Kujitolea Tanzania (TSV FOUNDATION) limefanya ziara ya kitaaluma katika Taasisi ya Elimu Tanzania - TET kwa lengo la kujifunza kwa kina kuhusu mtaala ulioboreshwa wa elimu kuanzia ngazi ya elimu ya awali hadi elimu ya juu. Mafunzo hayo yameongozwa na Kaimu mkurugenzi Taasisi ya Elimu Tanzania Bw. Moses Ziota.
Kaimu mkurugenzi Taasisi ya Elimu Tanzania Bw. Moses Ziota, akiomgoza mafunzo.
Mwenyekiti wa Shirika Mwl. Juma Hamisi alianza kwa kutoa historia na majukumu ya shirika kwa Kaimu mkurugenzi Taasisi ya Elimu Tanzania Bw. Moses Ziota, pamoja na kamati nzima ya wakufunzi.
Mwenyekiti wa shirika akieleza historia fupi na majukumu ya shirika
Katika ziara hiyo, washiriki walipata fursa ya kuelewa mabadiliko muhimu yaliyoboreshwa katika mtaala, mbinu mpya za ufundishaji na ujifunzaji, pamoja na namna bora ya kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya dunia ya sasa.
Mafunzo ya mtaala ulioboreshwa
Aidha, wakufunzi wa Taasisi walitoa mchango mkubwa katika mafunzo haya kwa kuwasilisha kwa ufanisi andiko la mtaala ulioboreshwa pamoja na sera mpya ya elimu, jambo lililoongeza uelewa mpana kwa washiriki wote.
Tunathamini mchango mkubwa wa Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kutoa maarifa na uzoefu unaotuwezesha kuona nafasi yetu kama wasomi katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Shirika linatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Taasisi ya Elimu Tanzania kwa ushirikiano wao, mapokezi mazuri, na uwezeshaji wa ziara hii muhimu.
Kwa pamoja, tunaendelea kujenga kizazi chenye maarifa, ujuzi na maadili bora kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.
Mwisho: shirika litaendelea kuwajengea uwezo walimu Kuwa mahiri katika taaluma ya ufundishaji.
#Elimu bora, Haki ya kila Mtanzania
No comments:
Post a Comment