TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA SHIRIKA


 Shirika linapenda kuujulisha umma kuwa Mkutano Mkuu wa Shirika ulifanyika kwa mafanikio makubwa tarehe 21 Februari, 2026 katika Ukumbi wa mikutano Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Posta-Dar es salaam.

         Mkutano huo uliwakutanisha wanachama wa shirika, viongozi pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo na uendeshaji wa shughuli za shirika. Katika mkutano huo, washiriki walipata fursa ya kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za shirika kwa kipindi kilichopita, kujadili mipango ya maendeleo ya baadaye pamoja na kutoa maoni na mapendekezo ya namna bora ya kuimarisha utendaji wa shirika.


 Aidha, mkutano ulijadili na kupitisha maazimio mbalimbali yatakayosaidia kuimarisha shughuli za shirika, kuongeza ushirikiano kati ya wanachama na wadau, pamoja na kuendeleza malengo na dira ya shirika katika kuhudumia jamii.


Uongozi wa shirika unapenda kuwashukuru wanachama wote, wadau na washiriki wote waliohudhuria mkutano huo kwa mchango wao wa mawazo, ushiriki na ushirikiano wao katika kuhakikisha mkutano unafanyika kwa mafanikio.


Shirika linaendelea kuwakaribisha wadau wote kushirikiana nalo katika kutekeleza mipango na miradi mbalimbali yenye lengo la kuleta maendeleo chanya katika jamii.


Mwisho, shirika linatoa shukrani za dhati kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima - TEWW kwa kuendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na shirika letu katika kutekeleza shughuli na malengo yanayolenga kuleta maendeleo chanya katika jamii. Ushirikiano huu ni muhimu katika kuhakikisha tunafanikiwa kufikia malengo yetu ya pamoja.


"ELIMU BORA, HAKI YA KILA MTANZANIA"

No comments:

Post a Comment